Baadhi ya wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wakichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka wa fedha 2019-2020 ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Baadhi ya Mafundi mitambo na Watangazaji wa Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC wakiweka mitambo sawa ili kuhakikisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019/2020 ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar inasikika na kuonekana vizuri kwa Wananchi
Mkurugenzi wa Elimu ya Sekondari wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Bi Asya Iddi Issa (wa kwanza kushoto), akibadilishana mawazo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma pamoja na Naibu Waziri wa Wizara hiyo Mhe Simai Mohammed Said kabla ya kuingia ndani ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Unguja.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma (wa kwanza kushoto) akiwa na mtoto anaelelewa katika nyumba ya kulelea watoto Mazizini, baada ya kumaliza futari ya pamoja na watoto hao iliyoandaliwa na mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein iliyofanyika jana ndani ya nyumba ya kulelea Watoto Mazizini Mjini Unguja.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma akiwa na Naibu Waziri wa Elimu wa mwanzo kulia Mhe Simai Mohammed Said, nyuma yake ni Naibu Waziri wa Ujenzi na usafirishaji Mhe Mohamed Ahmada wakiwa katika Picha ya pamoja na wanafunzi kutoka Skuli mbalimbali waliofika Baraza la Wawakilishi Zanzibar kusikiliza Hotuba ya bajeti ya Wizara yao.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakiwapa hongera Waziri wao Mhe Riziki Pembe Juma na Naibu Waziri Mhe Simai Mohammed Said, mara baada ya kuwasilisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2019-2020 katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Chukwani Mjini Unguja.
Naibu Waziri wa Afya Mhe Harusi Said Suleiman akisikiliza muendelezo wa mashindano ya kuhifadhi Qur-aan, ambapo alifika kwa niaba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe Riziki Pembe Juma, yaliyofanyika katika msikiti wa Ijitimai Kidoti Mkoa wa Kaskazini Unguja.